Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Mu’min Al-Rifa‘i, mshauri wa uhusiano wa kidiplomasia wa Lebanon, katika taarifa yake alisisitiza kuwa kuweka kawaida kwa mahusiano si tu usaliti kwa Umma, bali ni usaliti na kuhatarisha uwepo wetu, na hili ni jambo ambalo hatutalikubali kamwe.
Alisema: Sisi tuko juu ya ahadi ya Katibu Mkuu wa Hizbullah, shahidi Sayyid Hasan Nasrallah, na tumejifunga na ahadi yake na tunailinda turathi yake. Tunashikamana na muqawama na silaha zake; muqawama huu uliotoka ndani ya watu kama mwitikio dhidi ya ubeberu wa Magharibi na uhalifu wa Kizayuni–Kimarekani, ambao uhalali wake, uamuzi wake na irada yake ni irada ya watu wa Lebanon kutoka katika makabila, madhehebu na maeneo yote.
Sheikh al-Rifa‘i aliongeza kuwa: Kwa wale wanaopigia debe kuwa na mahusiano ya kawaida na Israel, tunawaambia kuwa kuweka kawaida si tu usaliti kwa Umma, bali ni usaliti na kuhatarisha uwepo wetu, na hili ni jambo ambalo hatutalikubali; na baada ya kurithi turathi ya ushindi, heshima na utu, hatutakubali kusalimu amri wala kunyenyekea.
Alibainisha kuwa yeye (al-Rifa‘i), pamoja na Mahdi Mustafa, msimamizi wa jalada la uhusiano wa kisiasa katika Chama cha Kiarabu cha Kidemokrasia, walishiriki katika mkusanyiko ulioandaliwa na harakati ya “al-Nasr” mbele ya kaburi la Sayyid Hasan Nasrallah. Katika mkusanyiko huo walihudhuria wawakilishi wa vyama na nguvu za Kilebanoni, Kipalestina, Kiislamu, Kiarabu na Kinasser, na taji la maua likawekwa juu ya kaburi lake.
Maoni yako